Sera ya Faragha
Ilisasishwa mara ya mwisho: Oktoba 2026
Sera hii inaeleza jinsi Lumenlabs ("sisi") inavyokusanya, kutumia na kulinda taarifa unapotumia DaftariDuka au tovuti ya daftariduka.com.
1. Taarifa tunazokusanya
- Taarifa za akaunti: jina la duka, barua pepe, nywila (iliyosimbwa/hashed), na jukumu lako kwenye mfumo (mfano: mmiliki au muuzaji).
- Taarifa za biashara unazoingiza mwenyewe: bidhaa, bei, idadi ya bidhaa dukani, mauzo, ankara, malipo, wateja na matumizi.
- Taarifa za kiufundi za msingi: muda wa kuingia na kutoka kwenye mfumo, kwa ajili ya usalama na utendaji.
2. Jinsi tunavyotumia taarifa
Taarifa zako zinatumika pekee kuendesha huduma ya DaftariDuka kwa duka lako: kuhifadhi mauzo yako, kutengeneza ripoti zako za hesabu, na kukusaidia unapohitaji msaada. Hatuuzi taarifa zako kwa kampuni nyingine.
3. Mahali data yako inapohifadhiwa
Data ya duka lako inahifadhiwa kwenye hifadhidata ya DaftariDuka iliyoko kwenye seva yetu, si kwenye simu yako. Hii ina maana unaweza kuingia kutoka kifaa chochote — simu au kompyuta — na kuona data ile ile. Pia ina maana unahitaji mtandao ili kutumia mfumo.
4. Nani anaweza kuona data yako
Ufikiaji wa data unadhibitiwa kwa akaunti na majukumu (users, roles na permissions). Ni watumiaji uliowaruhusu wewe mwenyewe kwenye duka lako wanaoweza kuingia. Wafanyakazi wetu wa kiufundi wanaweza kufikia data pale tu inapohitajika kutatua tatizo la kiufundi au kwa ombi lako.
5. Uhifadhi wa data (backups)
Tunafanya nakala za hifadhidata mara kwa mara kuzuia upotevu wa data. Tunaendelea kuboresha usalama wa nakala hizi, ikiwemo kuzihifadhi nje ya seva kuu.
6. Haki zako
Unaweza kuomba nakala ya taarifa zako, kuomba zifutwe, au kufunga akaunti yako wakati wowote kwa kuwasiliana nasi. Ukifunga akaunti, tutafuta data ya duka lako kutoka kwenye mifumo yetu inayotumika.
7. Wasiliana nasi
Maswali kuhusu sera hii au taarifa zako: WhatsApp +255 62 121 9695 au barua pepe nelson@lumenlabs.co.tz.
Tukibadilisha sera hii, tutasasisha tarehe iliyo juu ya ukurasa huu na, kwa mabadiliko makubwa, tutakujulisha moja kwa moja.