Msaada
Hapa utapata hatua za kuanza, majibu ya maswali ya kawaida, na namna ya kutufikia moja kwa moja.
Kuanza kutumia DaftariDuka
- Fungua programu. Nenda app.daftariduka.com kwenye kivinjari cha simu au kompyuta yako.
- Ingia kwenye akaunti yako. Tumia barua pepe na nywila uliyopewa au uliyojisajili nayo.
- Ingiza bidhaa zako. Moja moja, au pakia faili la bidhaa zote kwa mara moja.
- Anza kuuza. Kila mauzo yanaingia kwenye daftari lako na kujijumlisha yenyewe.
Maswali ya kawaida
Nahitaji mtandao?
Ndiyo. DaftariDuka inahifadhi data ya duka lako kwenye seva yetu, hivyo unahitaji
mtandao ili kuingia na kuuza. Faida yake: unaweza kuingia kutoka simu au kompyuta
yoyote na kuona data ile ile.
Je, naweza kutumia kwenye simu?
Ndiyo. Fungua app.daftariduka.com
kwenye kivinjari, kisha chagua "Add to Home screen" ili ionekane kama programu
ya kawaida kwenye simu yako.
Nimesahau nywila yangu.
Tumia kiungo cha "Forgot Password" kwenye ukurasa wa kuingia, au wasiliana
nasi kwa WhatsApp na tutakusaidia kuirejesha.
Wafanyakazi wangu wanaweza kutumia pia?
Ndiyo. Unaweza kuwaongeza kama watumiaji wa duka lako, na kuamua kila mmoja
aone nini. Wasiliana nasi tukusaidie kuweka majukumu yao.
Data yangu iko salama?
Data ya duka lako inafikiwa tu na watumiaji uliowaruhusu, na tunafanya nakala
(backups) mara kwa mara. Soma zaidi kwenye Sera ya Faragha.
Unahamia kutoka toleo la zamani? Kama ulikuwa unatumia DaftariDuka ya zamani kwenye simu yako na una mauzo ambayo hayajapanda kwenye mtandao, wasiliana nasi kabla ya kufuta programu ya zamani — tutakusaidia kuyahifadhi.
Wasiliana nasi
Tunajibu kwa Kiswahili au Kiingereza. Tuandikie wakati wowote: